Wednesday, April 20, 2011

wana wa bongo fleva

Mtu mzima Bob Junior aka Mr. Chocolate Fleva aka Rais wa Masharobaro leo mchana aliibuka mjengoni Clouds FM kwenye kipindi cha XXL na kusema kuwa kuna watu watatu wanaomtishia maisha na amewachukulia RB yao. Watu hao aliowataja kwa jina la Diamond aka Rais Wa Wasafi, Shetta pamoja na Meneja wa Shetta anaitwa Shabaha.
RB hiyo ambayo amewachukuli watu hao inasomeka hivi: OB/RB/6303/2011, baada ya kusikiliza vile nilijaribu kumcheki meneja wa msanii Shetta anayeitwa Shabaha na akaniambia kuwa na yeye kasikia hivyo so ameshangazwa kwa kitendo hicho na wala yeye hajui lolote.
 anajulikana kama d knob kwa sasa ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la mr sahani. wadau tumpe sapoti ya kutosha mwana ni mkali kwa sana tu sema ndio vile kubana kwingi kwa media nyingine kama wanaomba kazi. aminia mtu mzima

No comments:

Post a Comment